- poor 1
- poor 4
- poor 6
- poor 5
- mzee-ojwang

Katika taaluma ya sanaa wasanii wengi wanawafurahisha mashabiki wao lakini ndani ya  mioyo yao wanasumbuka sana na hata kimaisha wanang'ang'ana ili kupata cha kuwakimu.

Hii hapa orodha ya wasanii walioaga dunia wakiwa maskini.

1.Papa Dennis

Kifo chake Papa kiliwashangaza wengi baada ya mwili wake kupatikana eneo la pangani jumamosi usiku, Dennis ametoka katika jamii ya  umaskini hadi kuwa mtu mashuhuri kabla ya mkataba wake kuisha na Sadat.

Baadaye alifurushwa katika nyumba ambayo alikuwa anaishi na kuhamia katika studio moja Pangani, ambapo alionekana kuwa mwenye mawazo mengi.

Kwa bahati mbaya alipatana ameaga kwa kile inasemekana kuwa aliruka kutoka gorofa ya 7.

2.Achieng Abura 

Alifariki mnamo tarehe 20 Octoba 2016 katika hospitali kuu ya Kenyatta, kabla ya kifo chake Achieng aliomba mchango ambapo watu wawili au watatu walijitokeza na kusema hawana hela.

Akiwa katika mahojiano alisema kuwa aliitisha mchango ili kumpeleka mwanawe ng'ambo  akatibiwe na watu wakajitokeza na kumsaidia.

Baada ya kifo chake kila rafiki yake alitaka kutajwa japo wakati walipohitajika hawakujitokeza hata

3.Njenga Mswahili

Mcheshi huyo aliyekuwa akifanya kazi katika churchill show aliaga dunia 2019 Novemba kwa njia tatanishi pia.

James Anthony Njenga almaarufu Njenga Mswahili alifahamika sana kwa ucheshi wake wa lugha ya kiswahili kisha kupewa jina mswahili.

Mwili wake ulipatikana eneo la reli Dagoretti kwa kila inasemekana alikuwa na msongo wa mawazo kabla ya mauti yake.

4.Joe Kadenge

Shujaa huyu wa mpira aliaga dunia alipokuwa katika hospitali ya Meridian mjini Nairobi,mwanawe Oscar akizungumza kuhusu kifo chake alisema afya yake ilikuwa imedorora kwa muda mrefu.

Iliilazimu bima ya afya yakitaifa NHIF kulipa milioni ya katika hospitali aliyokuwa amelazwa kutokana na umaskini uliokuwa umemkumba.

5.Mzee Ojwang

Kwa waliozaliwa miaka michache iliopita wanatambua kama mzee Ojwang aliyekuwa mwigizaji bora na mcheshi katika onyesho la Vioja Mahakamani.

Kwa mara nyingi aliigiza wakiwa na mama kayayi na  aliaga dunia kwa kutokana na ugonjwa wa   nimonia.

Kabla ya kuaga kuna wakati alipoteza kuona na kisha NHIF ikamlipia hospitali ili apate matibabu.

View Comments