- Rungu 1
- giedeon na Rungu
- gideon and raymond

Seneta wa  Baringo na mwanawe rais mstaafu Marehemu Daniel Moi leo amepewa rungu ya Mzee Moi ili kumpokeza jukumu la kuiongoza familia ya Moi kisiasa . Kakake mkuu Raymond Moi ambaye ni mbunge wa Rongai ,alimkabidhi Gideon Rungu hiyo akisema sasa ndiye atakayekuwa na jukumu la kuipa familia ya Moi   mwelekeo wa kisiasa .

Hatua hiyo huenda ikatafsiriwa kama  kumpepeza Gideon katika kilele cha usemi katika jamii ya wakalenjin. Gideon  na naibu wa rais William Ruto wamekuwa katika  nipe nikupe ya kujaribu kuchukuwa uongozi wa jamii hiyo kisiasa lakini baada ya uchaguzi  wa 2013 ambapo Ruto aliungana na Uhuru Kenyatta kuunda serikali ,amechukuliwa kama ‘kiongozi’ wa wakalenjin kisiasa . Wakati wa hafla fupi ya kumpa Gideon Rungu hiyo Raymond amesema –

‘KWA  VILE MZEE   ALITULINDA ,NA KULINDA KENYA VIZURI ,TUNAAMBIA HUYU(Gideon) KANU IAMKE.. NA TUKO NA BBI ,WE WANT TO  BE PART OF IT..WE SUPPORT BBI’  amesema Raymond .

Alipoichukua rungu hiyo ,Gideon aliahidi kufanya kadri ya uwezo wake kufaulu katika jukumu lake la kuiongoza familia ya Moi kisiasa .

‘HATA KUSHIKA HII RUNGU…ANYWAY…NITAJARIBU ..NIKIWEKA MWENYEZI MUNGU MBELE,MENGI TUTASEMA BAADAYE’. Amesema Gideon .Kakake

View Comments