Mapenzi ya usaliti; Wasanii na watu mashuhuri waliopatikana wakiwasaliti na kusalitiwa na wapenzi wao
Wasanii na watu mashuhuri wanahitajika kuwa kioo cha jamii katika macho ya watu wengi haswa wakiwa ni mashabiki wao wanaowaenzi ,lakini kinaya ni kuwa wengi wao wamewapa wadanganya wapenzi wao kwa muda mrefu na hata kukana madai ya kuwa mipango ya kando hata wakipatikana wanakataa.
Hawa hapa waliosalitiwa na kusalitiana licha ya wao kuwa wasanii na watu mashuhuri;
Ben Githae
Ben alimsaliti mkewe kwa kuwa katika uhusiano na mwanamke mwingine na kumpachika mimba kisha kujifungua watoto mapacha, ambapo alikiri kuwa ni ukweli alimsaliti mkewe.
Susumila
Mkewe alimpa talaka mwaka wa ,2014 huku akidai kuwa ana macho ya mapenzi kwa wanawake wengine, Susumila alifahamika sana kupitia wimbo wake wa 'Hidaya'
Gloria Muliro
Ni mwamuziki ambaye anafahamika sana kwa sanaa yake ya uimbaji, na pia kuimba nyimbo akiwashirikisha wasanii mbalimbali humu nchini.
Gloria alisalitiwa na mumewe waliokuwa wamefunga ndoa na yeye Eric Omba, ilidaiwa kuwa Erick alikuwa anawachumbia wanawake wengine katika kanisa lake ,jambo lililompelekea Gloria kutalakiana na yeye.
Kenrazy
Ni msanii ambaye ameimba nyimbo tofauti,habari zake za kumsaliti mkewe zilichapishwa sana mwaka wa 2013, huku mashabiki wakitoa hisia nyingi kuhusiana na kitendo hicho.
DJ Crème De La Crème
Usaliti wake huwezi saulika katika akili za mashabiki wake, kwa kuoneka katika filamu akiwa amemsaliti mkewe bali na hayo aliomba msamaha na maisha kuendelea kama kawaida.
Diamond Platnumz
Ni mwanamuziki ambaye hawezi saulika katika vinywani vya mashabiki na watu wake kwa kumsaliti mkewe Zari.
Bali na kutoa nyimbo zake Diamond amekuwa katika mitandao ya kijamii kwa mambo tofauti.