1-4

Wakati wa sasa kila kitu kinafanyika katika mtandao wa kijamii, hata kuchumbiana ni jambo ambalo limekuwa katika mstari wa kwanza katika mtandao wa kijamii.

Si mtandao wa Facebook,twitter,instagram na hata kwenye mtandao wa youtube, wanapochumbiana kwanza mmoja wao anapaswa kutuma picha ili wazungumze.

Baadhi ya sababu ambazo watu wengi huenda katika mtandao wa kijamii nikama vile zifuatavyo;

Ni nafuu

Watu wengi hawapendi kutumia pesa zao visivyo faa wala kutumia kwa watu ambao hawajafamiana vyema,Hii inawezesha kuchumbiana katika mtandao wa kijamii kwa sababu hautumii pesa zozote.

Lakini wengi wanasema ukitaka kitu chema gharamia ili ukiona akichezewa na mwingine uone hio gharama na kumkumbatia hasiende.

Uoga

Si wote ambao wanawataka wachumba wananguvu ya kuwaambia uso kwa uso wanapokutana, lakini endapo utaandika ujumbe wako hapo uoga unaisha na kujieleza kwa undani.

Inafahamika sana katika dunia

Mwanaume anaweza kuwa katika nchi nyingine na anamchumbia mwanamke wa nchi nyingine kwa sababu wamejuana kupitia mtandao wa kijamii

Hawana wakati

Watu wengi hawana wakati wa kuenda na kuchumbiana ana kwa ana kwa sababu wamo katika shughuli zao na wanafanya kazi tofauti.

Inafanya kazi

Si mmoja au wawili ambao wamepata kipenzi cha maisha yao kupitia mtandao wa kijamii, na wanafunga ndoa na wanaishi pamoja bila ugomvi wowote.

Ni salama

Si wote ambao wanachumbiana katika mtandao wa kijamii wana nia njema bali wengine wanataka kulipiza kisasi ili machungu ambayo wanapitia katika maisha yao yaishe.

Rahisi kupekejeng 

Iwapo unataka kupekejeng na huna ujasiri wa kumuambia mtu wengi huenda katika mtandao wa kijamii na kutafuta mtu ambaye anataka kupekejeng kama yeye na kwa hakika hawakosi.

Wamechoka kupatana katika mikahawa

Wamechoka  sana na kupatana na wachumba wao na kuwala pesa tu na mwishowe wanakataa na kuwaruka mita mia moja.

Na wengi wamechoka kupatana na wao na mwishowe wanawaomba waende kupekejeng ilhali ni mara yao ya kwanza kupatana na wao.

Swali langu kwako ni je ni vyema kuchumbiana kupitia  mtandao wa kijamii?

View Comments