Kakake Nicki Minaj ahukumiwa miaka 25 jela kwa kumbaka binti yake wa kambo.
Kakake msanii wa Marekani Nicki Minaj Jelani Maraj, atasalia jela kwa miaka 25 baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka binti yake wa kambo mwenye umri wa miaka 11 .Jaji amesema Maraj ‘ameharibu’ mtoto huyo . Jaji Robert McDonald amesema Maraja anastahili adhabu hiyo ua miaka 25 jela kwa sababu alimbaka mtoto huyo mara kwa mara .
“ ULIMBAKA HUYU MTOTO .ULIMBAKA MARA KWA MARA’ amesema jaji Mcdonald
Kakake mwathiriwa alishuhudia Maraj alimdhulumu dadake na kawaambia maafisa wa shule yake .Nicki Minaj hakuwa kortini siku ya jumatatu ili kuwa na kakake mkubwa .Maraj aliiomba mahaama kumpa msamaha akisema kwamba hakuekeleza kitendo hicho .
“ NINGEPENDA KUOMBA RADHI KWA MACHUNGU NILIYOSABABISHA .NILIKUWA NA TATIZO LA KUNYWA POMBE KUPINDUKIA NA NAOMBA MSAMAHA KUTOKA KWA KORT’ Alisema Maraj .
Kabla ya hukumu hiyo kutolewa mwathiriwa ambaye ni binti yake wa kambo aliambia mahakama kwamba dhulma hizo zilimfanya kutaka kujiua .
“ SIKUFIKIRI NINGEMALIZA SIU KABLA YA KUPATWA NA KISA CHA KUTAKA KUJIANGAMIZA .NILIHISI KWAMBA SIKUWA NA SAUTI’
Jelani Maraj ameshtumiwa kwa kumbaka mara kadhaa binti yake wa kambo katika boma la familia ya Baldwin. Maraj alikanusha madai hayo akisema madai hayo ni wongo yaliyolenga kumpunja dadake Minaj,pesa .