patanisho.kulia

Gidi amefichua kuwa mara kwa mara yeye na mtangazaji mwenza, Ghost hulia ndani ya studio katika kitengo cha patanisho ambacho hujia kwako kila siku asubuhi.

Kitengo hiki huwaleta wawili pamoja ambao wamekosana na wanataka kurejesha uhusiano baina yao, haswa wanandoa ambao wanahisi kuwa ndoa yao inasambaratika.

Akizungumza nasi katika mahojiano ya moja kwa moja Gidi alisema kuwa patanisho ambayo imekuwa hewani kwa kipindi cha miaka saba sasa imegusa na kubadilisha maisha ya watu wengi.

 "Patanisho stories are every day problematic. Sometimes we have very funny stories while other days we have sad ones," alisema.

Gidi aliongeza akisema kuwa watu wanapitia changamoto nyingi katika mahusiano yao.

"Some are so touching that we also at times find ourselves crying in the studio. Some even make us go silent in the studio because they are sad.

There are other people who we try to reconcile but are just crying on air and so we also find ourselves crying. Others complain about why they are brought on the radio. I mean it is different always," alisema.

Tulipomuuliza jinsi kitengo hicho kilipozaliwa, Gidi alisema ilimchukua miaka mitano kupata wazo hilo.

"I tried so many ideas but then after five years of trying, we got Patanisho which was motivated by people calling in sharing their problems with us," alisema.

Akiongeza kuwa sasa hivi mamilioni ya watu wanafahamu patanisho.

"For the last seven years, it has grown immensely but it has been a lot of work behind the scene and building trust with people so they can be free to open up to you.

We make them feel free with us and that is why many are free with us. Another reason why the segment is loved is that it is clean and that there is no vulgar language used.

Anasema kuwa tuzo kuu kwake ni wakati yeye na Ghost wanapofanikiwa kuwapatanisha wapendanao.

Isitoshe kinacho mpa furaha zaidi ni wakti mmoja anapopiga au kutuma ujumbe akisema kuwa walipatanishwa na sasa hivi wanaishi kwa furaha.

Gidi alimalizia akisema kuwa bado ana enjoy taaluma yake ya radio na anapangia kuendelea kuwatumbuiza wakenya hadi siku atatosheka.

View Comments