Size 8 alieleza jinsi mwendazake mamake alimkubali Dj Mo awe mume wake, alizungumza na kusema kuwa wanaume wengi walitaka kumuoa lakini wakati ambao alimpeleka DJ Mo kwa mamake alimuambia atakuwa mume mzuri katika maisha yake.

"Sikumjua lakini nilipenda uaminifu wake,nilipopatana na yeye hakuwa na pesa lakini aliniambia hana pesa za kunionyesha wakati huu lakini maishani nitakuwa nazo." Size 8 Alisema katika mahojiano.

Aliongeza na kusema kwa kweli ni ngumu sana kupata mtu mwaminifu lakini alimchagua.

Licha ya DJ Mo kuwa hakuwa na pesa za kutosha  mkewe alisema alikuwa na lengo kuu katika maisha yake na alikuwa anataka mwanaume kama huyo.

" Ingawa nilisita kukaa na yeye alinionyesha jinsi alivyokuwa tayari kuwa na mimi." Alisema Size 8.

DJ Mo alipoulizwa kwanini alitaka kuanzisha familia na mkewe Size 8 alisema kuwa hakufurahishwa na umaarufu wake.

"Ni ngumu sana kujua mwanamke kamili." Aliongea.

Size 8 aliongeza na kusema kuwa walikula kiapo kuwa hawatazingatia sana maneno ya wakosoaji, pia alisema wao uomba sana kwa sababu umaarufu huja katika maisha ya mtu kwa ajili njia tofauti na maoni tofauti.

" Kejeli hazijawahi fanya ndoa yetu iwe katika msukosuko, wakati zilituadhiri ni wakati uja uzito wangu ulitoka mapema, ni jambo ambao lilitingiza imani yangu hadi nikakuwa mchoyo katika maisha yangu kwa maana nilitarajia mume wangu awe nami wakati huu mgumu lakini pia yeye alikuwa ameadhiriwa." Alisema Size 8.

View Comments