- Radio Queens
- massawe 2
- carol Radull 1
- kamene 1
- Terry Muikamba
- Linda
- Cate sidede
- Njoki Mburu

  Sauti zao zimesikiza kote katika redio kubwa za humu nchini . Kwa  ajili ya weledi wao na kuwepo kwa mitandao ya kijamii ,pia tumeweza kufahamu  sifa zao nyingine na hata tunaweza sasa kuunganisha sura na sauti ambazo husikika .Hawa hapa baadhi ya malkia wa redio wanaotesa masafa Kenya .

1.Massawe Japanni

Massawe ndiye mtangazaji wa Kiswahili naayefahamika zaidi kwa  kipindi chake ‘Bustani ya Massawe na hasa vitengo vya  ‘Ilikuaje’   na  ‘Dead Beat’ .  Amewavutia wasikilizaji wake kwa sauti yenye mkwaruzo mzuri na pia kicheko che bezo ambacho kinatupa tabasamu . Massawe ni mwanaharakti wa mtoto wa kike na aghalabu msimami yake huwa ya kuwatetea wanawake katika kila hali . Iwapo Radio Jambo ingekuwa ‘Kingdom’ Massawe angekuwa malkia wake .

  1. 2.Carol Radull

Huyu ndiye Malkia wa soka nchini . Kataa kubali ,hapajatokea mwanadada  katika utangazjai nchini ambaye ana ufahamu wa masuala ya soka kama CR. Ucheshi wake wakati  wa  kipindi cha The Score  katika Vituo vya  Classic 105  na  Kiss FM  kila jumamosi  ni baadhi ya  vinavyowavutia sana mashabiki wa soka nchini . Carol pia amekuwa nguzo muhimu sana miongoni mwa watangazaji na wadau wa spoti nchini waliozua  msisimko mpya miongoni mwa mashabiki wa soka nchini kwenda viwanjani kuvishabikia  vilabu vya humu nchini . Kando na ufahamu wake kuhusu soka ya ulaya ,CR pia hajakimya kuwakosoa wadau wa soka na waunda sera kwa kufelisha mchezo wa soka na fani nyingine za spoti nchini . Ujasiri wake kusema jinsi mambo yalivyo umemweka katika ligi nyingine ya  uanahabari/uanaharakati.

3.Kamene Goro

Mvuto wake hakuna asiyeujua .Mengi yamesemwa kumhusu lakini ukakamavu wake  umeshuhudiwa akisema kila kilicho fikrani mwake bila kujali matokeo . Mtangazaji huyo mwenye  uzito  wa alivyopewa hajachelea kuvuruga mitandao kwa picha zake zake ambazo aghalabu huwaacha wanaume wengi wakidondokwa.Anapiga kipindi cha asubuhi  ‘Morning Kiss’ pamoja na   dume  jingine lenye uzushi  Andrew Kibe.

  1. Terry Muikamba

Mashabiki wake wa  Kituo cha Classic wanamfahamu kama  Miss Sunshine.Mtoto wa kike  ana sauti nzuri na upole wa kuvutia lakini kama hujawahi kumuona anavyotembea kwa  msukumo wake wa kimahaba basi hujafika . Hutangaza pamoja na  Toto la Kiume  ,Mike Mondo,  ambaye  wanadada  hawatosheki na sauti yake .

  1. Linda Nyangweso

Sauti yake nzuri na lahaja ya kipekee ya lugha hii ya wenyewe imewavutia wengi sana . Ni Mwanadada mtulivu  lakini mcheshi pia .Ni mtu siyeweza kubanwa na anasema kilicho kizuri na ukimkosea pia utakipata .

  1. Cate Sidede

Cate  Sidede ni wa kipekee! Sauti nzuri na ukarimu usikadirika .  Mtangazaji huyu ni mseto wa urembo na akili. Amekuwa akipiga show  ya  mid-morning  kuanzia saa nne asubuhi hadi saa tisa  mchana katika Kiss Fm lakini sasa ameanza maangamizi katika kituo cha Smooth Fm .

7.Njoki Wa Mburu

Huwezi kuikosa  tabasamu ya Njoki wa Mburu hata kupitia sauti yake . Njoki ni mtangazaji wa kituo cha lugha ya kikuyu cha Gukena na kwa  sasa anapiga kipindi cha asubuhi pamoja na Kajim. Huenda usiweze kusikia lugha hiyo akitangaza lakini ukiisikia sauti na ucheshi wake Njoki,utataka kumpa muda wako .Ni mwanadada mkarimu sana na pia  nguzo muhimu sana kwa wasikilizaji wake kuhusu masuala ya kidini/Kiroho. Jumbe zake katika  mitandao ya kijamii huwa za kuwapa wafuasi wake matumaini  ya kuamini na pia himizo la kutenda mazuri .Njoki wa Mburu ni dhahabu kwa utangazaji wa lugha ya Kikuyu .

 

View Comments