hosi-pic

Watu watatu wamelazwa katika hospitali ya Murang'a baada ya kuonyesha dalili za kipindupindu, Afisa mkuu wa afya  Joseph Mbai alisema kuwa watu hao ni msichana wa miaka kumi na wanaume wawili.

Mbai pia alisema watatu hao wanatibiwa katika wadi za kipekee ili wachunguzwe zaidi kama wanaugua kipindupindu.

Aliongeza kusema kuwa wagonjwa hao wamekuwa wakiugua kuendesha na kutabika lwa muda sasa lakini wamo katika hali thabiti.

Mmoja wa wagonjwa ni eneo la mjini slum, mwingine ametoka eneo la Kayole na wa mwisho ni wa kijiji cha Wango mbai alisema.

Joseph pia alisema maafisa wa afya wametumwa katika familia za wagonjwa hao ili kufanyiwa mafusho.

"Tumewakubalisha baadhi ya maafisa wa afya kutembelea maeneo ambayo yameadhiruwa ili kubaini kiini cha ugonjwa huo." Alisema Mbai.

Aliwasihi na kuwauliza wenyeji wa vijiji hivyo pia waweze kuchemsha maji yao ya kunywa ili kuzuia ugonjwa huo.

Wizara  ya afya pia imesema kuwa itasimamsha uuzaji wa vyakula ambavyo si visafi, na pia kukomesha watu ambao wanaingia katika kaunti hiyo bila ruhusa huku wakiwapigia maafisa wa afya waliokuwa katika likizo simu ili warejee kazini.

Mwaka wa 2015 watu wawili waliaga dunia kwa sababu ya ugonjwa unaotokana na maji katika  kijiji cha Kabati kaunti ndogo ya Kandara.

Mwaka wa 2017 watu zaidi ya watu hamsini kutoka kijiji cha Kiunyu kaunti ndogo ya Gatanga  walilazwa hospitali kwa sababu ya ugonjwa huo.

Serikali ya kaunti hiyo imetoa njia mbalimbali ili kuzuia ugonjwa huo kuenea sana na watu wasiweze kuugua.

View Comments