bonga

NA NICKSON TOSI

Mzalishaji wa mziki katika kampuni ya Konde' Music Worldwide  Bonga alitangaza mapema wiki hili kuwa ameachana na kampuni hiyo inayomilikiwa na msanii Harmonize kwa kile alisema ni kutoelewana.

Akizungumzia swala hilo ,Bona aliongezea kuwa aliamua kwenda kuanzisha kampuni yake ya kutoa miziki baada ya kupata ustadi wa kuzalisha miziki .

Aliongeza kwa kusema hana tatazi lolote na Harmonize na ameondoka katika kambuni yake na baraka tele.

Bonga aliongeza kuwa wakati wowote ambapo Harmonize atajihisi kufanya kazi naye ,atakuwa tayari.

“Ninachoshukuru Mungu kwa Harmonize sijagombana naye nimeondoka nikamwambia Bro ni wakati wangu kufanya movement kwa sababu ya mitikasi maisha lazima yaendelee akaniambia freshi akanibless. Akitaka kufanya kazi akinitafuta tutafanya,”alisema Bonga.

“Nafanya sasa na Lykos Empire na sababu zangu za msingi ni kama msanii sasa. Nimeamua kusign niznze kutoa kazi zangu kama msanii… sikuwa nafanya kazi na Harmonize tu ila nimekuwa producer ambaye nimekulia katika himaya ya Konde Gang ila kwa sasa sipo pale. Nimeamua kufanya movement na kampuni nyingine kuanzisha maisha yangu mapya. Kila siku inatakiwa mtu uangalie kila hatua unazopiga,” aliongeza Bonga.

Baada ya Bonga kutia saini na kampuni nyingine ya kuzalisha miziki 'Lykos Empire'pamekuwepo na usemi kuwa hawakuwa wanapatani na mdosi wake Harmonize.

View Comments