KENEI

Afisa wa polisi Kipyegon Kenei huenda aliuawa.

Maafisa wa ujasusi waonaochunguza kifo cha afisa huyo wa polisi aliyekuwa akihudumu katika afisi ya naibu rais WilliamRuto wanaamini kwamba huenda Kenei hakujiua kama ilivyokuwa imedaiwa. Wanajaribu kuunganisha msururu wa matukio kubaini kwanini simu ya Kenei ilionekana kuondolewa mahali ilipokuwa punde tu baada ya kumpigia mkewe na kama alipokea au kumpigia mtu mwingine simu.

Maafisa wa DCI wanaendelea na harakati za kufuatilia vile simu hiyo ilizunguka. Afisa wa ujasusi aliyezungumza na Radio Jambo alisema kwamba Kenei alimpigia mkewe simu saa tatu na dakika 41, Februari 18 akiwa nyumbani kwake. Mazungumzo hao yalidumu dakika 53.

Wakitumia teknojia maalum ya kufuatilia mazungumzo ya simu baada ya kumtumia mkewe ujumbe, polisi wamebaini kwamba simu hiyo ilibadilishwa mahali ilikuwa mwanzoni hadi mahali pengine mtaani Imara Daima na sio nyumbani kwake Villa France House.

Teknokojia hiyo pia ilipata mahali simu yake ilikuwa wakati akituma shilingi 35,000 kupitia akaunti yake ya simu ya Benki ya Equity saa sita na dakika 25 usiku wa Februari 19.

“Kuzungushwa kwa simu hiyo kupitia maeneo mbali mbali hasa tofauti ya takriban saa mbili na nusu kati ya saa tatu na dakika 52 na saa sita na dakika 24 ni muhimu sana katika kubaini kilichofanyika,” afisa wa DCI alisema.

Wakati wa kutumwa pesa kwa mkewe zikiwemo shilingi 10,000 alizotumia babake, Kenei hakujibu jumbe kutoka kwa mkewe alipoulizwa kuhusu kiasi cha pesa kisicho cha kawaida alichokuwa amemtumia mkewe na babake. Simu yake ilizimika mwendo wa saa moja unusu asubuhi Februari 19 huku akaunti zake zote za mitatandao ya kijamii pia zikifungwa.

Kenei alifanya kazi katika ghorofa ya pili ya Jumba la Harambee House Annex ambapo kuna afisi ya naibu rais William Ruto. Alitarajiwa kuandikisha taarifa kwa idara ya DCI kuhusiana na uchunguzi wa zabuni ghushi wa silaha za kijeshi ya takriban shilingi bilioni 40. Uchunguzi huo unamhusisha aliyekuwa waziri wa michezo Rashid Echesa.

Echesa na washukiwa wengine wanasemekana kufanya mkutano katika afisi ya naibu rais kujadili zabuni hiyo bandia. Wakati huo mwanapatholojia mkuu wa serikali Johansen Oduor jana alisema kwamba huenda maafisa wa polisi walihitilafiana na eneo la uchunguzi katika nyumba ya chumba kimoja alimoishi marehemu Kenei.

View Comments