Shame on KDF: Tazama unyama ambao wanajeshi wawili walimfanyia kijana huyu huko Sotik
Polisi huko Sotik katika kaunti ya Bomet wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio ambalo wanajeshi wawili wa Kenya army wanashtumia kwa kumshambulia mwanamme mmoja na kumjeruhi vibaya.
Kamanda wa polisi katika eneo hilo Francis Nganga amesema tuko hilo lilifanyika katika kijiji cha Chebole siku ya jumatano .Kulingana na Nganga wawili hao Solomon Langat na Leonard Kirui wanaohudumu mombasa na Garissa mtawalia walimvamia Geoffrey Korir mwenye umri wa miaka 25 katika kituo cha kibiashara cha Chebole alipokuwa akienda nyumbani .Nganga amesema wanajeshi hao wamekimbilia mafichoni baada ya unyama wao . Nganga amesema uchunguzi wa mwanzo umeonyesha kwamba wanajeshi hao walikuwa wakilewa mchana kutwa katika eneo moja la burudani katika sehemu hiyo .
Korir alikuwa akielekea nyumbani mwendo wa saa tano usiku baada ya kutazama mechi katika kituo hicho wakati wanajeshi hao walipomshambulia . Haijabainika kilichosababisha wawili hao kumshambulia na kumjeruhi vibaya raia ambaye hakuwa amejihami wala kuwafahamu . Nganga amewataka wenyeji kuwa watulivu akiahidi kwamba wanajeshi hao wawili wataadhibiwa kwa kukamatwa na kufikishwa kortini kwa hatia ya kumshambulia na kumjeruhi raia .
Naibu mwenyekiti wa jamii ya wafanyibiashara katika eneo la chebole John Kirui amesema wawili hao wana tabia ya kuwahangaisha raia wakati wanapokuwa nyumbani kwa likizo na kujigamba kwamba hakuna atakayewafanya lolote kwa sababu wao ni wanajeshi .
" Hatuna amani wakati wawili hao wanapokuja nyumbani .. ni watoto wetu lakini wanatushambulia wakisema polisi hawawezi kuwakamata’ amesema .