Katika kitengo cha Story za Ghost Mulee, mtangazaji huyu mcheshi aliwaacha wengi wakiangua kicheko baada ya kusimulia kisa kimoja cha kushangaza kilichotokea nchini Nigeria.

Kulingana na Ghost, mhasibu (accountant) mmoja nchini humo aliwashangaza wengi baada ya kupatikana katika sakata ya ufujaji wa pesa.

Mhasibu huyo kwa jina Philomena Chiesa, alijipata matatani baada ya mkaguzi wa kifedha kubagua kuwa kitita cha millioni kumi hakibainiki kiliko katika shirika analofanyia kazi.

Na alipoulizwa fedha hizo ziliko alijitetea akisema kuwa kuna nyoka ambaye alimeza zile fedha zote, huku akiwaacha wengi na butwaa.

Soma usimulizi wake Ghost Mulee,

Wajua nchi ya Kenya na Nigeria kuna vitu kadhaa ambazo zafanana, kwa mfano hapa kuna EACC ya kupigana na ufisadi, Nigeria kuna EFC.

Kuna accountant anayejulikana kama Philomena Chiese na auditors walipofanya hesabu ikabainika kuwa millioni kumi hazijulikano ziliko.

Alipoulizwa mwanadada yule alisema kuwa fedha zile zimeliwa na nyoka.

"Nimeambiwa na mfanyikazi wangu na mfanyikazi mwenza kuwa zile fedha zimeliwa na nyoka, na sijui mnacho zungumzia kwani nyoka ilimeza fedha zote." Alisema yuke mwanadada.

Mwanadada yule kwa sasa amekamatwa na uchunguzi unaendelea.