gire Ali

Mfanyikazi wa KQ Ali Gire ambaye  amesimamishwa kazi kwa kupiga picha ya video na kuisambaza ndege ya China Southern Airlines ikitua katika uwanja wa JKIA  ikiwa na abiria 239  siku ya jumatano sasa amesema maisha yake yamo hatarini .

Wakati ikitangaza kumsimamisha kazi KQ ilimshtumu kwa kukiuka sera za kampuni kutokana na jinsi alivyoshughulikia tuki hilo baada ya video yake kuonyesha raia wa China wakiwasili nchini licha ya hofu ya uwezekano wa kuleta virusi vya Corona Kenya .

Video hiyo iliwafanya wakenya kuhamakishwa na hatua ya serikali kulichukulia suala hilo kwa wepesi huku matifa mengi duniani yakipiga marufuku  safari za ndege kuingia nchini mwazo ili kuzuia usambaaji wa virusi hivyo. Siku ya ijumaa ,Ali alithibitisha kwamba amesimamishwa kazi huku wengi mtandaoni wakimtetea na kulaani hatua ya KQ  kumfurusha kazini .

View Comments