- Abortion-696x379
- unnamed

Kamwe shilingi mia Tano haitoshi kwetu sisi!,Wakaazi wa Tharaka Nithi walisikika wakisema baada ya kupewa shilingi hizo ili wahudhurie mkutano wa BBI utanaofanyika katika kaunti ya Meru .

Walinena haya wakikejeli kitendo hicho kwa maana walikuwa wamehahidiwa shillingi elfu tatu.

"Tumenyanyaswa Kabisa. Shilling mia tano si ya kulipa mwananchi kutoka Chuka hadi meru..na tunashindwa tumekuja kufanya nini Meru." Mmoja wao alisikika akiongea.

Mwingine alisikia akisema kuwa hata mtoto wao  hawezi lipwa shillingi mia tano tu licha ya wao kutoka maeneo mbalimbali ili kuhudhuria mkutano huo.

Wakaazi hao walionyesha pesa hizo wakinung'unika na kusema kuwa ni heri tu warudi wakajishughulishe na kazi zao badala ya kuharibu wakatii wao wakiwa katika eneo hilo.

"No way, turudini humu nje tuanze kutafuta riziki na tuweze kuhustle." Mmoja wao Alisema.

Mwanaume mmoja alijitokeza na kusema kuwa walikuwa wamehaidiwa elfu tau lakini matakwa yao na makubaliano hayajatimizwa.

"Kutoka Chuka mpaka hapa ni Sh300. Nimebaki na Sh200. This will not be enough." Mmoja Alizungumza.

Walipokuwa wakizungumza na kulalamika, watu wengi walifurika katika uwanja huo na kusema kuwa pia wanataka wapewe ripoti ilio kwenye BBI.

Wengine walisema kuwa wamechanganyikiwa na hawajui chochote kuhusu BBI na kusema kuwa viongozi wamekuwa wakihahirisha matakwa yao na wanataka leo kujieleza na kueleza uoga wao katika mkutano huo.

Mkutano huo umepangwa baada ya kinara wa ODM Raila kupatana na viongozi waMt Kenya.

Viongozi hao walikutana na kinara huyo katika ofisi yake na kumueleza mipangilio ya mkutano wa Februari,29.

View Comments