unnamed

Mia tano pekee? Siwezi kuchukua !

Ndio kauli ya baadhi ya wakaazi wa Tharaka Nithi ambao walilipwa shilingi 500 ili kwenda Meru kwa mkutano wa BBI katika uwanja wa Kinoru ."Tumenyanyaswa Kabisa. Shilling mia tano si ya kulipa mwananchi kutoka Chuka hadi meru..na tunashindwa tumekuja kufanya nini?’  mmoja amesikiza akisema

Mwingine alisema ‘ Hata mtoto wako huwezo kumpa 500’. Wakati kundi hilo likionyesha  noti za shilingi 500 zilizotolewa ili walipwe  ,wengine walisema heri werejee  kufanya kazi zao .  Vijana waliokuwa wamejikusanya kabla ya kulipwa wamesema walikuwa wameahidiwa shilingi 3000 na wameshangaa kupewa 500 ."Kutoka Chuka mpaka hapa ni Sh300. Nimebaki na Sh200.  Hii haitoshi’ mmoja amesema .

Huku umati ukikusanyika katika uwanja wa Kinoru ,wakaazi wametaka kupewa nakala za ripoti ya BBI  wakidai kwamba viongozi wamekuwa wakibadilisha msimamo kuhusu yaliyomo katika ripoti hiyo na sasa wamewakanganya .

View Comments