Ni kama Movie! Mama Diamond amzuia Tanasha kuondoka TZ na mjukuu wake Naseeb Junior
Sarakasi imezuka na sasa filamu ipo huko bongo baada ya msanii Diamond Platinumz na mpenzi wake Tanasha Donna kutengana .
Uvumi unazagaa kwamba Tanasha alipata habari kwamba Simba alikuwa yungali na tabia za kulala na wanawake wengine nje ya uhusiano wao na hata akathibitisha . Katika posti ya hasira Tanasha amemtaja Diamond kama ‘shetani’ na mtu ambaye hana utu ndani yake . Tazama .
Baada ya hapo alifungasha virago vyake na alikuwa akipanga kuondoka . inaibuka kwamba mamake Diamond Sandra hakumtaka Tanasha aondoke akiwa na mtoto wa Diamond Naseeb Junior .
Udaku kutoka Tanzania waarifu kwamba palitokea kizaazaa kati ya mama Dangote na Tanasha kuhusu mtoto huyo mwenye umri wa miezi mine . Aliandika baadaye katika mtandao
“TIME TO SAY GOODBYE & GOD BLESS YOU ALL.”
Tanasha kwa sasa yuko Nairobi na haijulikani endapo atawahi kusafiri tena kurudi Tanzania