- tanzania
- magufuli

Shirika la soka nchini limewaagia wachezaji kutosalimiana kama ilivyo ada wanapocheza kadanda.

Kulingana na masharti tuliyoyaona, shirika hilo liliwakataza wacheza kutosalimiana kabla ya mechi kuanza jambo ambalo linajulikana duniani kote.

Hata hivyo, wachezaji wameshauriwa kutumia lugha ya ishara kama nji mbadala.

"Utaratibu wa wachezaji kupeana mikono kabla ya kuanza mechi hautatumika kwa sasa, na badala yake watasalimiana kwa ishara tu," maagizo hayo yalisema.

Utekelezaji huo utakuwa katika mechi za ligi kuu ya Vodacom na ligi zingine kuu nchini humo.

Jumanne, Magufulu alihakikisha hajasalimia wageni wake kwa mikono katika ikulu.

Badala ya kushikana mikono, rais Magufuli alionekana akitumia miguu kumsalimu Maalim Seif Sharif Hamad.