bbbb

NA NICKSON TOSI

 Msanii Bahati ambaye pia ni meneja wa lebo ya EMB amezungumza kwa mara ya kwanza kuelezea ni kwa nini hazungumzi tena na mama wa kambo aliyemlea baada ya kumpoteza mamake mzazi.

Akizungumza wakati wa kipindi chake kwenye televisheni moja humu nchini, Bahati alisema kuwa mamake huyo wa kambo na mwanawe Benjamin walimuita kama mtu anayeabudu shetani yaani Devil Worshiper.

Kulingana na Bahati, wawili hao waliafikia kusema hayo baada ya kuwatembela Yatta akiwa na gari tofauti, hali iliyomfanya mamake huyo wa kambo kusema eti alikuwa anataka kumtoa kafara mwanawe.

“Mimi nilireach out kwa familia, mama Benja that was like 4 years ago nilikuwa naenda namchukua vile tu Mungu amenibariki Kenya ikaanza kunijua kidogo. Akikuja nampeleka juu sina pesa enough hadi anaona Uhuru Park, anaona town. Mimi sikuwa hata na gari nilikuwa nachukuanga car hire natoka hapa nadrive mpaka Yatta naenda namchukua na sasa juu uko na car hire kesho ukimuendea unaenda na gari tofauti so the next thing nilipigiwa juu pia shida ingine nilikuwa nayo sijui kama ni shida ama ni nini most of the time juu naimba mpaka late, mimi huamka kama 3AM kuomba sasa si unajua huyu mtoto ako excited anamuambia kuhusu Nairobi kurudi home vile aliambia mamake vile Bahati ako na gari nyingi alafu anaombanga na nguvu saa tisa mamake akanipigia akaniambia mimi ni devil worshiper, mimi mwenyewe hata sijui devil ana worshippiwa pande gani. Ikakuwa ati nataka kusacrifice brother yangu hapo ndio mimi nilicut communication,” alisema Bahati.

Bahati alisema kuwa alikuwa anaamka asubuhi na mapema majira ya 3am kuomba swala ambalo nduguye wa kambo aliliona kama lisilo la kawaida.

View Comments