IMG_1375

Leo katika studio tulikuwa na pacha wa mwendazake Papa Dennis alinayefahamika kama Papa D almaarufu Papa Simon, kutufahamisha  jinsi alivyojua kifo cha ndugu yake.

"Tulikuwa kwenye studio na papa tulikaa kwa muda bila kumuona, saa nne usiku tulipigiwa simu na kuambiwa twende chini kuna jambo ambalo limetendeka

Tulipokimbia chini tulimpata ndugu yangu amelala chini akiwa anapumua kidogo na anatoa damu kwa mapua, tulikuwa hapo mimi, ringtonena mjukuu

Tulionyeshwa jinsi mtu ameanguka kutoka katika ghorofa ya pili uwa anakaa hananga sura kabisa mbali Papa sura yake ilikuwa sawa

Naweza kusema ndugu yangu Papa aliuawa hakujiuwa, lakini uchunguzi humo mikononi mwa DCI na atatupatia matokeo hivi karibuni." Simon Alieleza.

Simon alisema kuwa Papa alikuwa anawasaidia watoto wa dadazake ambao sasa ni yeye anayewajibikia majukumu hayo.

Alikuwa na haya ya kusema kumhusu mwendazake.

"Papa alikuwa na mawazo mengi kwa sababu ya pesa ambazo alikuwa amedai lebo aliokuwa awali, nami nilimwambia asiwe na mawazo mengi

Aliniambia anawadai zaidi ya laki 500, Papa hakuwa na maadui. ndio alikuwa na amesongwa na mawazo lakini hakuwa mtu wa kujiuwa." Alisema Simon.

Kwa sasa wamebaki ndugu wawili ambao mmoja wao ni muhubiri.

Simon alisema kuwa kulingana na upasuaji wa mwili Papa hakujiuwa.

"Nashukuru Nairobi chapel na nyumbani kwetu kwa kutushikilia wakati huo mugumu, naingia katika usanii ili kuendeleza ndoto za ndugu yangu

Nimekuwa na wasiwasi kwa maana sijajuwa hasa nini kilimuua kaka yangu." Simon Alisimulia

Kwa mengi zaidi tembelea mtandao wa kijamii wa youtube." Aliongea.

View Comments