Wakili anayefanya kazi katika kaunti ya Nakuru hii leo ameshtakiwa kwa njama ya mauaji ya raia wa Ubelgi aliyefahamika kama  Dysseller Mireille Lesoipa almaarufu Leila.

Inadaiwa wakili huyo aliungana na kundi ili watekeleze kitendo hicho,John Gakinya alikana madai hayo mbele ya mahakama hii leo.

Kati ya mwaka wa 2018 Desemba na Julai,2019 John aiungana na wengine ambao hawakuwa mbele ya mahakama na kupanga njama ya kumuua Dysseller.

Alikana madai hayo na kusema hana hatia mbele ya hakimu Daniel Ogembo.

Polisi hawajapata mwili wa mwendazake ambaye wanaamini aliuawa ilhali John ameshtakiwa kwa mauaji hayo, Dyseller alipotea mapema mwaka jana na polisi wanaamini kuwa kundi la watu lilikuwa na njama ya kumuua ili warithi mali zake.

Ilidaiwa Gakinya alisalimisha kesi mahakamani ambapo Lucy Waithera ambaye ni rafiki wa mwendazake na mfadhili wa wasia wa uongo wa mwendazake.

Pia kulikuwa na cheti cha kifo cha uongo ambacho ni cha mwendazake Mireille.

Waithera rafiki wa karibu wa mwendazake alienda mbele ya mahakama kwa mara ya kwanza lakini hakuja mahakamani kwa mara ya pili kwa maana ripoti ya tathmini ya akili yake haikuwa tayari.

Ripoti ya Gakinya ilikuwa tayari na alikuwa wa kwanza kushtakiwa katika mauaji hayo, kesi yake itaendelea jumatatu wiki ijayo ili ajulishwe vile ata lipa dhamana yake.

Mshtakiwa huyo aliambia mahakama kuwa watapinga dhamana yake ya kuahiliwa huru.

  
View Comments