tanasha

Kumekuwa na tetesi mitandaoni kuwa Tanasha amemshtaki aliyekuwa mpenziwe, Diamond, kisa na maana; Kwa kumpotezea wakati.

Tanasha kwa upande wake alidhibitisha kuwa hana mipango yoyote ya kulipwa Fidia ya aina yoyote na Diamond.

Hii ni kinyume na habari zilizoenea kuwa baada ya kutengana kwao, Donna alimshtaki Diamond akidai kuwa staa huyo alimpotezea muda wa miaka miwili.

Iwapo hili ni ukweli, Tanasha atakuwa akifuata nyayo za staa wa Marekani Mariah Carey aliyemshtaki mpenziwe kwa kumpotezea wakati na akapewa Fidia ya milioni 50.

Tangia kutengana kwao, Tanasha amekuwa akijaza miotandao yake na jumbe za kujipa moyo na amekuwa akishambuliwa na mashabiki wakimrai kusahau yaliyopita na kuganga yajayo.

Hata hivyo, habari hizo kuwa anapania kumshtaki Diamond ni kama zilimfikia na alitumia mtandao wake kukana madai hayo akisema;

“Too much FAKE NEWS

out here! Let me make it

clear that there is NO

court case or whatever it

is thats being said out

there!

Can a giri live her Iife in

peace? Can we just focus

on the right & positive

things? Tha fuuuuu‍♀️”

View Comments