Rais Uhuru Kenyatta  amezitaka benki na kampuni za simu kupunguza gharama ya  malipo yanayotozwa kufanya ununuzi wa bidhaa kutumia simu na kadi  huku taifa likikabiliana na visa viwili zaidi ya maambukizi ya virusi vya Corona .

Uhuru siku ya jumapili amesema afisi za serikali ,biashara na kampuni zinafaa kuzingatia kuwaruhusu baadhi ya wafanyikazi wake kufanyia kazi nyumbani isipokuwa wale wanaohitajika kwenda afisini . Hatua hiyo inadhamiria kuzuia  usambaaji wa virusi hivyo kupitia pesa zinazopokezana kwa watu . Wakenya wamehimizwa pia kuepuka maeneo yaliyo na watu wengi  na kupunguza mikutano kama vile hafla za makanisani ,harusi na maazishi.

‘Epuka maeneo ya duka za jumla ,maeneo ya burudani na kupunguzo mrundiko wa watu katika magari ya usafiri wa umma  kadri ya uwezo wake’ rais amesema .

Serikali pia imepiga marufuku usafiri  wa kuingia na kuondoka nchini  nan i wakenya walio na paspoti pekee  ndio watakaoruhisiwa kuingia nchini  endapo watpatikana na virusi hivyo na kuwekwa katika wadi maalum  kwa matibabu na uangalizi .

View Comments