Nyota wa filamu Idris Elba apatikana na virusi vya Corona
Muigizaji maarufu wa fialamu na msanii wa muziki muingereza Idrissa Akuna Elba al maarufu Idris Elba ndiye mtu wa hivi punde maarufu kupatikana na virusi vya corona .
Katika video aliyoweka mtandaoni ,akiwa pamoja na mkewe Sabrina Dhowre, Elba amesema alipimwa na kupatikana na virusi hivyo. Hata hivyo amewatuliza mashabiki wake akisema hana daalili za ugonjwa huo na alijitenga alipogundua kwamba kuna uwezakano alitangamana na watu
Aliandika;
https://twitter.com/idriselba/status/1239617034901524481
Idris Elba aliendelea kueleza umuhimu watu kunawa mikono na kuepuka mikutano ya hadhara huku ulimwengu ukiendelea kupambana na mkurupuko wa virusi hivyo .zaidi ya mataifa 30 ya afrika yameripoti visa vya ugonjwa huo huku kenya ikisajili visa takriban vinne hadi kufikia sasa