NA NICKSON TOSI

Rais Kenyatta hii leo ameanda hotuba  chini ya wiki moja ili kuarifu taifa kuhusiana na hatua ambazo serikali  imechukuwa wakati huu ambao taifa linakabiliana na janga la Corona.

Rais amewarai wakenya kuendelea kudumisha usafi akisema ndio njia ya kipekee ambayo inaweza kuwawezesha kuepukana na virusi hivvyo.

Wakenya wenzangu ,ningependa muendelee vivyo hivyo na kuangazia haswa usafi kwa kuosha mikono kila wakatio kama njia ya kusaidia serkali kupigana na janga hili ambalo limetukumba kama taifa na mataifa mengine ulimwenguni.asliema rais Kenyatta

Rais vile vile  aliwaonya wanaofanya biashara katika maduka ya kijumla wanaopania kuongeza bei ya bidhaa maradufu akisema atakayepatikana basi serikali haitakuwa na la kufanhya bali kuwachukulia hatua.

Kwa wenzetu ambao mnafanya biashara nchini,huu si wakati wa kuongeza bei ya bidhaa ili kupata faida ,ni hatia kutumia wakati kama huu ambapo serikali inakabiliana na janga la Corona na wewe unatumia fursa hiyo kuongeza bei ya bidhaa,nina kuambia iwapo tutasikia duka lolote ama lalama zozote ,basi tutakuchukulia hatua na kufunga biashara zako,aliongeza rais.

Rais Kenyatta aidha amehofia kuwa huenda sekta ya Utalii nchini itaathirika pakubwa kutokana na idadi ndogo ya watalii ambao wanawasili nchini.

Kenyatta amesema serikali inajaribu iwezavyo  kwa ushirikiano na wizara ya Utalii kuweka mikakati ili kuhakikisha kuwa uchumi wa taifa haurudi chini katika sekta hiyo muhimu ambayo inachangia pakubwa kwa ukuaji wa uchumi wa taifa.

Kwa sasa kutokana na Corona ,mnafahamu kuwa idadi ya watalii ambao walikuwa wanazuru nchini imepungua manake kiula mtua anataka kujitenge kivyake ili asiambukizwe ni virusi hivi,kama serikali pia tunajaribu kama tuwezavyo ili kuhakikisha kuwa sekta hii muhimu hairudi chini manake ndio kiinua mgongo cha uchumi wetu.Alielezea rais Kenyatta.

Hotuba ya rais inajiri siku moja tu baada ya waziri afya Mutahi Kagwe kutangaza kuwa taifa la Kenya lilikuwa limesajili mtu wa 4 aliyekuwa ameambukizwa na virusi vya Corona.

Kagwe aidha aliongeza kuwa watu 23 waliokuwa wamewekwa  chini ya karantini katika hospitali ya Mbagathi walifanyiwa vipimo vya matibabu na kupatikana hawana virusi hivyo na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Kufikia sasa mataifa takriban 123 ulimwengu yameathirika na mkurupuko wa Corona huku taifa la Italia likiwa ndilo lililoathirika pakubwa kutokana na idadi kubwa ya maambukizi na vifo vinavyoripotiwa nchini humo.

View Comments