chania cool

Mwanamme  mmoja mwenye  umri wa miaka 30 ameaga dunia ghafla baada ya kuanza kukohoa katika basi moja la kwenda Mombasa .

Polisi wanasema dereva wa basi hilo la kampuni ya Chania Cool  alripoti kwamba mmoja wa wasafiri katika basi hilo  Fred Mwakima alianza kukohoa walipokuwa wamesimama kwa muda katika hoteli ya  Taleh ,karibu na mtito Andei nakisha kuaga dunia muda mfupi baadaye .

Maafisa wa afya kutoka  kaunti ndogo ya Kibwezi wamelifukizia dawa basi hilo  na kuoondoa mwili wa msafiri huyo kutoka gari hilo . Licha ya serikali kuwaagiza watu kusalia nyumbani ,maelfu ya watu wangali wanakimbilia kwenda mashambani na kuhatarisha maisha ya walioko sehemu hizo za mashinani .

View Comments