NA NICKSON  TOSI

Gavana wa kaunti ya Machakos Alfred Mutua amepiga marufuku oparesheni ya boda boda katika kaunti hiyo kwa muda wa wiki mbili katika harakati za kukabiliana na virusi vya Corona.

Dr Mutua anadai huenda hatua hii itasaidia pakubwa kupunguza uwezekano wa usambaaji wa virusi hivyo.

Hatua hii inajiri wakati kaunti jirani ya Makueni imetoa agizo kwa wananchi kuichukua miili ya wapendwa wao  inayohifadhiwa katika hifadhi za maiti kwenye kaunti hiyo.

Gavana wa Makueni Kivutha Kibwana amewapatia wakaazi saa 48 kutekeleza agizo hilo ili kupunguza idadi ya watu katika hifadhi za maiti.

Kibwana vile vile amesema iwapo miili hiyo haitakuwa imechukuliwa baada ya muda wa makataa, serikali ya kaunti itachukuwa jukumu la kuzika.

Kaunti zingine zilizowaamuru wananchi kuchukuwa  miili ya wapendwa wao kutoka hifadhi mbali mbali ni Kisumu na Kakamega.

View Comments