- kagwe
- kmm

NA NICKSON TOSI

Waziri wa afya Mutahi Kagwe alidhibitisha kuwa watu 9 zaidi nchini wamepatikana na virusi vya Corona na kufikisha idadi ya watu walioathirika na virusi hivyo nchini kufikia 25.

Visa hivyo vipya vimeripotiwa kutokea katika Kaunti za Nairobi, Mombasa, Kilifi na Kwale huku watu 7 kati yao wakiwa wakenya na wawili wakiwa watalii.

Kagwe aidha alidhibitisha kuwa serikali imepokea ufadhili wa vifaa takriban 25,000 kutoka kwa mfanyabiashara Jack Ma ili kusaidia serikali kupigana na virusi hivyo.

Waziri aidha aliongeza kuwa watu 82 wamefanyiwa vipimo na wanasubiri kupata matokeo ya vipimo vyao.

Mutahi vile vile alisema serikali imefanikiwa kupata watu 745 wanaosemekana kukaribiana na watu waliothirika na 98 kati yao wameruhusiwa kwenda nyumbani.

Kagwe alitoa onyo kwa wakuu wa hoteli za humu nchini dhidi ya kuongeza malipo ya huduma zao akisema wale watakaopatikana watachukuliwa  hatua za kisheria. Waziri Mutahi alisema hapo jana kwamba serikali hii leo itatangaza mikakati zaidi ya kupambana na usambaaji wa virusi hivyo

View Comments