- quarantine
- Uhuru kenyatta

  Wakenya na viongozi   mbalimbali wamekuwa wakitoa maoni yao kuhusu hatua ambazo serikali inafaa kuchukua ili kuzuia usambaaji wa virusi vya corona .

Baadhi ya watu wamependekeza zuio kamili la kutotoka nje ili kuwazuia watu kutangamana na kuhatarisha uwezekano wa kusambaza virusi  hivyo. Tayari uwezekano wa kuwepo zuio kama hilo  limewafanya maelfu  kukimbilia mashambani na  wakati wa  kuandika hapa vituo kadhaa vya mabadi ya kwenda mashambani vimefurika watu wanaosafiri ambao wanahofia kupatikana jijini Nairobi wakati wa tangazo la kutotoka nje .

Mwanzo wengi wanatoroka jiji kwa sababu ya gharama ya maisha na uwezekano wa ongezeko la visa vya uhalifu endapo mfumo wa serikali na sheria utafeli endapo virusi hivyo vitakosa kuthibitiwa . Wakili Donal Kipkorir amesema katika twitter kwamba kwa sababu wakenya wengi wanaishi katika hali ya umaskini serikali haifai kutangaza tu zuio la kutotoka nje bila kujali watakavyojikimu kimaisha wakati wa muda huo .

Gavana  wa zamani wa Kiambu  William Kabogo amesema katika ujumbe wa video kwamba  serikali kwanza inafaa kuhakikisha kwamba wakenya wanapewa kinga dhidi ya gharama wanazolazimika kubeba wakati wa zuio hilo, huku akipendekeza kusaidiwa kwa waajiri kuwalipa wafanyikazi wao na wenye nyumba kuwapa msamaha wa kodi wapangaji wao .

https://twitter.com/honkabogo/status/1242697117354921987

Endapo zuio hilo litatangazwa kote nchini au katika baadhi ya kaunti basi picha hii inafaa kukupa  taswira ya matayarisho unayofaa kufanya na  vitu unavyofaa kununua .

Iwapo serikali itaichukua hatua hiyo basi wakenya ndio wanaofaa kujilaumu wenyewe kwa sababu jitihada za kujaribu kuwahamasisha kwamba virusi hivyo vinasambaa na wanafaa kusalia nyumbani au kuchukua tahadhari  hazijafua dafu . Waziri wa afya Mutahi Kagwe alighadhabishwa sana na mienendo ya wakenya hasa kuhusu tabia ambazo zinaonekana kuingiza mzaha katika vita dhidi ya  corona alipotaja uamuzi wa wazazi kuwapeleka wanao katika nyumba za walimu kwa mafunzo ya ziada na wahudumu wa matatu kuendelea kuwabeba abiria waliojaa katika magari ya usafiri wa umma .

View Comments