pjimage (10)

NA NICKSON TOSI

Baadhi ya watu maarufu wa humu nchini wanaishi katika makasri ya mabilioni zaidi ya Ikulu ya rais, jinsi tu wengine kutoka kwa mataifa ya kigeni wanavyoishi maisha yao ya kifahari.

Kama paparazzi tuko ange kukuonyesha baadhi ya nyumba wanazoishi baadhi ya watu hao wa humu nchini.

  1. Simon Kabu

Simon Kabu anakumbukwa na wengi kutokana na historia ya maisha yake yalivyokuwa kablya ya kufanikiwa na Mola .

Kwa sasa Kabu anaishi katika kasri linalokisiwa kuwa la Milioni 10 .

Kabu alianza kama makanga na kwa sasa ni mkurugenzi mkuu wa kampuni inayoangazia maswala ya usafiri nchini[tours and travels].

2. Jared Otieno

Mfanyabiashara huyu anayefahamika kutokana na namna anavyoishi maisha yake ya kifahari anaishi katika jumba la milioni 115 mtaa wa Karen.

Otieno vile vile anamiliki jumba lingine eneo la Lavington na inadaiwa alitumia milioni 100 kulijenga.

Jumba hilo la Karen liko na vyumba vya kulala 5, jikoni na kidimbwi cha kuogelea na vingine vingi.

3. Linus Kaikai

Mwanahabari huyu anamiliki jumba la kifahari eneo la Kajiado linalosemekana lilimgharimu mabilioni ya pesa kulijenga.

Ni miongoni mwa wanahabari wachache wanaomiliki majumba kama hayo nchini.

4. Yvonne Okwara

Anafahamika sana kwa weledi wake wa kusoma taarifa nchini.

Wasichokijua mashabiki wake ni kuwa mwanahabari huyu anamiliki jumba la kifahari katika jiji kuu la Nairobi na ni vigumu kumpata kama amepiga picha katika nyumba hiyo na kutundika katika mitandao ya kijamii.

5. Akothee

Msanii huyu kando na nyumba yake ya kifahari anayomiliki Mombasa, Akothee ana nyumba nyingine ya kifahari Rongo ambayo kwa wakati mmoja alinukuliwa akisema ataishi kwa nyumba hiyo wakati atakapostaafu kutoka kwa sanaa ya muziki.

Akothee pia anamiliki kampuni ya usafiri ama kwa jina travels company kwa jina Akothee Safaris.

View Comments