NA NICKSON TOSI

Taifa la Italia limekuwa likirekodi idadi kubwa ya vifo vya watu kila siku kutokana na virusi vya Corona ambavyo inadaiwa vimezambaa kaskazini mwa Italia na kuwaacha maelfu ya watu wakiwa wameambukizwa na wengine wengi wakiwa wamepoteza maisha yao.

Chini ya masaa 24 taifa hilo limeandikisha idadi kubwa ya watu ambao wamepoteza maisha yao takriban 969 kutokana na Corona ,huku mataifa mengine kama vile Uhispania ikiandikisha vifo vya watu 769 na Ufaransa ikiandikisha vifo 299 vifo hivyo vyote vikitokea chini ya masaa 24.

Kwa sasa mataigfa mengi Uropa yamejipata pabaya kutokana na virusi hivyo ambavyo chimuko lake ni Uchina.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani WHO maafisa wa afya zaidi ya 50 wameaga dunia katika taifa la Italia kutokana na Virusi vya Corona.

View Comments