- Boda
- Boda boda 3

Fred  Ndung’u  amejawa mawazo kupindukia na licha ya kujaribu kadri ya uwezo wake kusahau yanayompa usumbufu wa fikra ,hawezi kusahau kwa sababu hadi leo anatafita majibu ya jambo ambalo limemfika miezi sita iliyopita . Mke wake walimuacha na kutoroka na mhudumu wa boda boda!

Fred ni  karani katika afisi ya  ushuru ya kaunti moja nchini katika eneo la mlima Kenya na   amejipata na aibu sana kuwasimulia watu kwamba mke wake alimuacha yeye ambaye ana kazi inayoweza kutajwa kama nzuri na malipo  ya kuridhisha ili kwenda na mhudumuwa boda boda . Masaibu yake yalianza mwezi juni mwaka jana wakati mke wake ambaye alikuwa muuguzi alipomuandika kazi jamaa mmoja wa boda boda   katika mtaa wao ili awe akija kumchukua kazini wakati wa jioni na pia kumpeleka asubuhi na mapema . Fred hakuwahi kujiambia hata kwa sekunde moja kwamba uhusiano kati ya mke wake na mtu wa boda boda ungebadilika na kuwa kimapenzi ili kumtia katika hali anayojikuta sasa .

Baada ya muda wa miezi kadhaa wakati jamaa yule anambeba mke wake kwenda na kurudi kazini ,Fred alianza kugundua mabadiliko katika tabia yake mkewe lakini hakulitia maanani suala hilo .wakati walipokuwa wakifanya mazungumzo ,ghafla tu  mke wake angelitaja jina la Yule boda boda.

‘ Ngatia  ana mbuzi kadhaa wa maziwa na kuku ,unafaa nawe pia ufanye kilimo cha pembeni’ .Ni baadhi ya kauli ambazo  zingeponyoka  mke wa Fred ,Stella .

Walipoanza ugomvi , Stella angetoka nje na mtu wa kwanza kumpigia simu ili kumsimulia kilichofanyika alikuwa Ngatia ,jamaa wa boda boda . mwanzoni Fred hakujali kwa sababu alimdunisha Yule  Ngatia akishangaa mtu wa bda boda angemtishia nini sasa . Kumbe chake Chuma , na sio cha doshi kilikuwa motoni!

Ngatia alianza kutumia ule mwanya wa kuzuka malumbano ya mara kwa mara kati ya Fred  na Stella na kuanza kumtongoza . muda sio mref ,Stella alianza kuhisi kwamba maisha yake yangekuwa hata mazuri iwapo angeolewa na mtu kama  Ngatia ambaye alikuwa mpole ,hakupenda ugomvi na alikuwa mtu mcheshi sana . Yamkini maskini Fred alikuwa sasa kajitangaza kama shetani ,ukali wake  na majigambo ya kufanya kazi katika idara ya fedha ya kaunti yalimfanya asijione kama binadamu bali ,  mungu mdogo pale mtaani .

Kuna dhana kwamba watu wanaofanya kazi ya boda boda ni wahuni na hawana  mustakabali mzuri lakini dhana hiyo ni potovu  na ilimletea mashaka Fred .  By the time alipokuwa akifunguka macho ,Ngatia ,jamaa wa boda boda alikuwa ameingiza mizizi ya mapenzi katika nafsi ya Stella na walikuwa washapiga mipango yao .

Watu mtaani walianza kurusha matone ya uvumi hapa na pale ambyo mara nyingi Fred aioyaokota hasa katika kumbi kama vile sehemu za baa alikopeda kwenda kulewa siku za ijumaa na wikendi . Uvumi ulipowafikia mama mboga ktika masoko madogo madogo ya kuelekea mtaa wao,haikuwa siri kwamba jamaa wa boda boda sasa alikuwa akimsaidia Fred kulamba asalia yak wake nyumbani .

Kuna walioanza hata kumfanyia kejeli na kabla hajapandwa na mori ili kuweza kumuuliza mkewe kuhusu kilichokuwa kikisemwa ,  Stella na Ngatia walikuwa wamehama hadi katika mji wa Karatina baada ya Stella kufaulu kupewa uhamisho na idara ya afya ya kaunti husika . I say, msiowaone hawa jamaa wa boda boda mitaani na vijijini mkawachukulia kwa wadharau ,wanaweza kukupiga chenga na kukufanya hata uwalelee watoto wao,na mkeo!

View Comments