Corona Robot: Tunisia yatumia roboti kuwazuia watu kutoka nje.
Wizara ya usalama wa ndani ya Tunisia imeanza kutumia roboti za polisi ili kuwazuia watu kutoka nje baada ya serikali ya taifa hilo kutangaza marufuku ya kutotoka nje ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona .
Roboti hiyo kwa jina PGuard, inaendeshwa na maafisa walio katika sehemu ya mbali na inaweza kumtambua mtu aliye sehemu ya mbali kando na kuwa na kamera kadhaa.
Picha na sauti zinazochukuliwa na roboti hiyo zinawekwa katika tovuti ya wizara ya usalama wa ndani huku wanaokiuka agizo la kutotoka nje wakiulizwa maswali na roboti hiyo na kutakiwa kuonyesha vitambulisho vyao.
Tunisia imekuwa chini ya marufuku ya kutotoka nje tangia Machi tarehe 17 na mamlaka ziliweka masharti makali kuzuia usafiri wa watu kuanzia tarehe 22 machi .
Nchi hiyo imethibitisha visa 455 vya ugonjwa huo huku watu 14 wakiaga dunia. Raia wa Tunisia Anis Sahbani aliyetengeza roboti hiyo amesema iliundwa mwaka wa 2015 ili kufanya doria muhimu za usalama