04 April 2020 1 Min Read
Ligi ya primia yawataka wachezaji kupunguza mishahara kwa asilimia 30
by Davis Ojiambo Habari
NA NICKSON TOSI
Baada ya kufanya kikao na uongozi wa vilabu Ijumaa, usimamizi wa Ligi ya Primia ulipendekeza kuwa wachezaji wa vilabu vyote vinavyoshiriki katika ligi hiyo kukubali kupunguza mishahara yao kwa sasilimia 30, ikiwa ni njia mojawapo ya kuchanga pesa za kusaidia serikali kukabiliana na janga la Corona.
Taarifa kutoka kwa Premier league imesema kuwa ilikuwa inafahamu changamoto ambazo vilabu vinapitia wakati huu ambao ligi hiyo imesitishwa. kwa hivyo, kama njia ya kusadia wachezaji wengi kutopoteza ajira msimu huu ambao biashara nyingi zimefungwa ni vyema wapunguze mishahara yao.