Tokeni hapa ! Akothee afurusha binti zake kwa sababu ya Coronavirus
Msanii mpenda sakata Akothee amewafukuza wasichana wake wawili dakika chache tu baada ya kuwasili ili kumtembelea .
Mama huyo wa watoto watano alihamakishwa na hatua ya binti zake kutaka kumpiga hug ilhali walikuwa wamewasili kutoka uwanja wa ndege. Akothee aliamua kuwatoa mbio kwa kuwaitia mbwa wake wakali .
Kulingana naye, Rue Baby na Fancy Makadia walikuwa wamewasili na huenda wana virusi vya Corona kwani hata hawakuwa wameoga. Katika video alizoweka katika instagram Akothee ametishia kuwaitia polisi endapo hawataoga na kujitakasa na kuziweka nguo zao katika jik ili kuua virusi
“They said no hug, stay away from me you idiots, you have just come from the airport and you want to hug me, those airport sits have corona. Go away and shower and get into the swimming pool and disinfect yourselves or else I will call police on you,” Akothee alifoka .
Rue Baby anasisitiza kwamba alikuwa amenawa mikono lakini mamake hakutaka kusikiza hilo.
“Corona has no boundaries, it is real, it doesn’t know whether you are my mother or whatever, please don’t bring corona here,”
Alisema
Kwa wiki mbili zilizopita Akothee amekuwa nyumbani pamoja na mbwa wake akiwaburudisha mashabiki wake kwa video anazoweka mtandaoni .