Covid 19: Visa 16 zaidi vyaripotiwa na kufikisha jumla ya watu 142 walio na coronavirus nchini
Idadi ya visa vya watu walio na virusi vya Coronavirus sasa imefikia watu 142 baada ya watu 16 zaidi kupatikana na ugonjwa huo . visa hivyo vipya ni vya raia 15 wa Kenya na raia 1 wa Nigeria .
Katibu wa utawala wa Afya Mercy Mwangangi amesema visa hivyo 16 vimegunduliwa baada ya serikali kufanyia vipimo sampuli 530 katika saa 24 zilizopita. Serikali hadi kufikia sasa imewapima watu 3,836 .Mwangangi amesema kati ya watu 16, 11 wana historia ya kusafiri mara kwa mara kutoka nje ya nchi.
Visa tisa vimetoka katika maeneo ya karantini ilhali saba ni kutoka kwa watu ambao walitangamana na waliothibitishwa kuwa na virusi hivyo hapo awali . Ameongeza kwamba wanaofariki kwa ajili ya virusi hivyo watazikwa chini ya 24 .Hafla za maazishi yao zitawahusisha tu watu 15 wa familia zao
Mwangangi ameongeza kuwa watu wanaozuru maeneo ya watu wengi kama vile maduka ya jumla ,masoko ya wazi na wanaotumia usafiri wa PSV wanafaa kuvalia barakoa kila wakati ili kuzuia usambaaji wa virusi hivyo.