NA NICKSON TOSI

Naibu gavana wa Kilifi Gideon Saburi amepata pigo tena hii leo baada ya mahakama ya Mombasa kumrudisha kizuizini kwa siku 3 kufwatia hatua yake ya kukiuka amri ya Serikali .

Saburi atarudishwa katika mahakama hiyo ya Mombasa siku ya Jumatano kubaini iwapo atawachiliwa kwa dhamana au la.

Saburi alishtakiwa baada ya kukiuka amri ya serikali ya kujiternga kwa siku 14 baada ya kurejea nchini akitokea ziara yake katika taifa la Ujerumani.

Alilazwa katika Hospitali ya rufaa ya Mombasa baada ya kupatikana na virusi vya Corona

View Comments