- Donna 1
- donna 2
- donna 3
- donna 4
- donna 5

Tanasha Donna  amefichua mengi katika mahojiano aliofanya na   jarida la True Love .

Msanii huyo  alieleza mambo mengi yaliyofanyika katika maisha yake baada ya yeye na Diamond kuanza  uhusiano . Donna  alieleza kwamba mwanzoni mwa uhuisiano huo, mpango wake haukuwa kupata mimba  na Staa huyo wa muziki. Alifichua kwamba Chibu alitaka kumuoa baada ya kujuana naye kwa miezi mitatu  na alishangaa sana alipogundua kwamba alikuwa mjamzito .

”I was careful not to fall in love with him completely because I wanted to know him better. I was shocked to learn I was pregnant for him. I was not ready to be a mother. It happened because I was not keeping track of my menstruation cycle,”  alisema Tanasha

  Donna anasema baadaye alianza kufikiria kuhusu kuitoa mimba hiyo. Hata hivyo anasema licha ya kuwaza kuhusu fikra hiyo amefurahi hakuchukua uamuzi huo .

”I really thought of terminating the pregnancy and also promised myself to be more careful next time, should I have gone the termination way, but thank God I did not go through with my thoughts,” Tanasha  aliongeza

Kitu kizuri ambacho kiliibuka kutoka kwa uhusiano wake uliofeli na Diamond ni mtoto wao wa kiume aliyezaliwa Oktoba mwaka jana na kuitwa  Naseeb Junior.

 

Kulikuwa na madai kwamba Diamond hakufanya  rasmi  uhusiano wake na Donna  kwa ajili alishauriwa dhidi ya kumuoa mwanamuziki mwenzake kwani pangetokea ushindani .

 

Diamond amesalia kimya kuhusu kukatika kwa uhusiano wake na Tanasha  na itachukua muda kabla ya kufahamu  msimamo wake kuhusu kilichotokea .

View Comments