Mkewe Harmonize , Sarah amuandikia barua siku chache baada ya kumblock
Harmonize na mkewe wife Sarah Michelotti wameanza kuzua mhemko sasa. Siku chache baada ya kila mmoja kukataa kumfuata mwenzake katika mitandao ya kijamii, Sarah amemuandikia Hamornize barua
Kipusa huyo raia wa Italia aliamua kuchukua hatua ya kuandika barua hiyo ili kuthibitisha kwamba yeye na msanii huyo bado wapo katika ndoa. Kumekuwa na uvumi kwamba huenda Harmonize na kipenzi chake wametengana lakini Michelotti ametumia instagram kuwafedhehesha mahaters kwa kuiweka picha yake na Harmonize
Katika picha hiyo Sarah alieleza jinsi anavyothamini mume wake akiandika;
“The most expensive husband of my love. Always on point baby,”
Hii ni baada ya kulipuka madai kwamba Harmonize alimsaliti mkewe kwa kushiriki mapenzi na Nicole Berry aliyehusishwa katika video ya wimbo wa bedroom wa msanii huyo. Wiki iliyopita, imesambaza video mtandaoni inayoonyesha mwanamke anayedaiwa kuwa Sarah akifoka makali nje ya nyumba inayodaiwa kuwa ya Nicole Berry. Pia kumekuwa na madai kwamba Hamornize amekuwa akiishi na mwanadada huyo jambo ambalo lilimpa hamaki Sarah .
Sarah bado hamfuati Harmonize katika instagram lakini alimtag katika posti yake ya mapenzi. Hatua ya Sarah na Harmonize kuacha kumfuta kila mmoja katika insta ilizua hofu kwamba huenda ndoa yao ilikuwa imevunjika .