08 April 2020 1 Min Read
Kongamano la magavana lililotarajiwa kufanyika katika kaunti ya Makueni lafutiliwa mbali
by Davis Ojiambo Habari
- COG
- oparanya
NA NICKSON TOSI
Kongamano la saba la magavana nchini lililotarajiwa kuandaliwa katika kaunti ya Makueni kuanzia TareheĀ 20-23 Aprili mwaka huu limefutiliwa mbaliĀ kwa hofu ya Corona.
Kongamano hilo huwaleta pamoja viongozi wa serikali kuu na magavana wa magatuzi yote 47 nchini ili kujadili hatua ambazo serikali hizo za ugatuzi zimeafikia na changamoto ambazo zinakumba ugatuzi nchini.
Jumla ya watu 179 tayari wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona nchini Kenya. Hii sio hafla ya kwanza kufutiliwa mbali kutokana na janga la corona huku ligi mbali mbali za soka duniani zikisitishwa kutokana na hofu ya maambukizi ya corona.
MHARIRI: DAVIS OJIAMBO