‘Diamond alinipenda hivyo’ Wema Sepetu afichua mbona alinyoa nywele zote kichwani
Wema Sepetu ametambulika kwa jinsi alivyobadilisha muonekano wake mara nyingi, lakini hakuna aliyemtaraji kunyoa nywele zote na kusalia na kichwa kisafi miaka kadhaa iliyopita.
Wengi walishangaa ni kipi kilichomfanyikia ili kulazimu hatua kama hiyo. Hata palizagaa uvumi kwamba alishauriwa kunyoa nywele zote baada ya kumzuru mganga ili kumsaidia arudiane na Diamond
Kama kioja kweli, walirudiana baadaye na wakasahau tofauti zilizoibuka kati yao. Lakini Wema sasa amepasua mbarika kuhusu kilichomfanya kunyoa hivyo kwani anasema alipata uhuru wa kuweza kuosha kichwa chake alivyotaka.
Kupitia ukurasa wake wa instagram muigizaji huyo alisema;
ThrowBack Thursday…
#NiMwendoWaViparaaaaa
Ila kama ni kuthubutu jamani nilijuaga kuthubutu kwa kweli… Para Para kama ngozi… Afu nilikuwa naingia anywhere, anytime, anyhow… Nikioga naskia rahaaaa… Afu wakati huo aliekua mpenzi wangu akawa anakihusudu kipara pia basi mambo yakawa BullBull… Maisha haya….
MHARIRI: DAVIS OJIAMBO