NA NICKSON TOSI

Rais Uhuru Kenyatta Jumatano alijiunga na mamilioni ya wakenya ambao walituma risala za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na waliomjua mwanariwaya Ken Walibora kutokana na kifo chake cha ghafla ambacho kilitokea baada ya kugongwa na gari.

Kiongozi wa taifa amemtaja Walibora kama mtu aliyefanya kazi kwa umakini sana na aliyefanikisha ukuaji wa Kiswahili si katika taifa la Kenya tu bali katika bara zima la Afrika.

Rais vile vile amesema kazi za uandishi ambazo gwiji huyo wa Kiswahili alikuwa amezifanya zitasalia za maana na kumbukizi kwa vizazi na vizazi.

Walibora  wa miaka 56 aliripotiwa kupotea Ijumaa na jamaa zake na taarifa za kifo chake zilitangazwa Jumatano na kusemekana kuwa aligongwa na gari alipokuwa anatoka kazini.

Tanzia: Mwandishi Ken Walibora ameaga dunia

Miongoni mwa vitabu alivyokuwa ameandika ni kama Ndoto ya Amerika (2003), Kisasi Hapana (2009), Nasikia Sauti ya Mama (2015), Kidagaa kimemwozea, Siku Njema na nyingine nyingi

View Comments