Ambassador Kyle

Balozi wa Marekani nchini Kenya Kyle McCarter amewashauri Wakenya kujikinga kwa barakoa pamoja na kuzingatia masharti mengine ili kudhibiti janga la Corona.

Kupitia taarifa kwenye Twitter, McCarter amesikitika kuwa hadi sasa wakenya wengi hawatumii maski kujikinga kutokana na virusi vya Corona.

Aidha, balozi huyo aliwasihi wakenya kuzingatia tahadhari zilizotolewa na serikali kupitia Wizara ya Afya ili kuzuia usambazaji na maambukizi zaidi za Corona.

Hakuna kati yetu anayeweza kukadiria madhara ya homa hii ya Wuhan lakini tunafaa kuchukua tahadhari za kimsingi tunazozijua." McCarter alisema.

Aidha aliongeza kusema kuwa maagizo yaliyotolewa na serikali kuzuia maambukizi zaidi ya Corona yanafaa kutiliwa maanani kwa kuwa yatazalia kwa muda mfupi tu kabla maisha ya kawaida kurejelewa.

"Tutarejea kwenye mafanikio na utamaduni wetu wa kujumuika pamoja  hivi karibuni." alisema.

Hili kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona, serikali imewashauri Wakenya kujikinga kwa maski kwenye maeneo ya umma pamoja na kukaa mbali mbali na wenzao.

Kwa sasa visa vya maambukizi  ya Corona vimefikia 281, idadi ya waliofariki kutokana na virusi hivyo vikifikia 14 huku Wakenya waliothibitishwa kupona wakiwa 69.

View Comments