nigerian mother

Mwanamke mwenye umri wa miaka 68 huko Nigeria amejifungua mapacha  katika  Hospitali ya mafunzo ya chuo kikuu cha Lagos(LUTH)

Aliekewa mimba kutumia njia ya kisayansi IVF.

Wasiu Adeyemo,  kutoka hospitali hiyo amesema  mwanamke huyo alikuwa  akipata mimba kwa mara ya kwanza

Bwana Adeyemo amesema mwanamke huyo alijifungua kupitia njia ya upasuaji tarehe 14 Aprili  baada ya kuibeba mimba yake kwa wiki 37 .

Ameongeza kwamba, yai la uzazi la mwanamke huyo lilitundikwa katika eneo tofauti na alikojifungulia mwanamke huyo

 

View Comments