SEX+WORKER

NA NICKSON TOSI

Wafanyabiashara 24 wa ngono katika kaunti ya Makueni ni miongoni mwa watu 37 waliopelekwa kwenye karantini ya lazima baada ya kukiuka amri ya serikali ya kutokuwa nje majira ya usiku.

Maafisa wa polisi kutoka kituo cha Emali waliwatia mbaroni wakiwa na wateja 6 Jumatatu jioni wakiwa nje kinyume na sheria zilizowekwa.

Sikio la Kufa halisikii dawa! Wanawake 39 watiwa mbaroni kwa kuhudhuria harusi kisiri

Msako huo pia uliwatia mbaroni wahudumu wa nyumbani ama mbochi wakiwa barabarani wakiuza pombe.

Watu hao wote sasa wanaendelea kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Emali wakisubiri kupelekewa katika shule ya wasichana ya Mulala kwa karantini ya lazima.

Wakenya hawana maskio kamwe! Watu 25 watiwa nguvuni wakinywa mvinyo

Kamishna wa polisi kaunti ya Makueni Farah Maalima amewataka maafisa wote wa polisi kaunti hiyo kuwa ange na kuwatia mbaroni watakaokiuka sheria.