Vijana 21 watiwa mbaroni wakirekodi video za ngono, Nakuru
NA NICKSON TOSI
Vijana 21 katika kaunti ya Nakuru walitiwa mbaroni na maafisa wa usalama wakiwa katika harakati za kurekodi video za ngono.
Walionaswa ni wavulana wanane na wasichana 13.
Sikio la Kufa halisikii dawa! Wanawake 39 watiwa mbaroni kwa kuhudhuria harusi kisiri
Inadaiwa vijana hao walisajiliwa kutoka shule za upili na vyuo vikuu na kuwekwa kwenye kikundi cha Whatsapp, hii ni kuambatana na ripoti iliyothibitishwa na polisi.
Katika siku hiyo ya kiama, walikutwa na maafisa wa polisi wakiwa kwenye klabu moja vyungani mwa nyumba za mtaa wa Milimani mjini Nakuru na kulingana na polisi hawakuwa kwa umbali wa mita 1 kama ilivyopendekeza serikali.
Maafisa wa polisi pia wameanzisha uchunguzi kuhusiana na ripoti kuwa huenda raia mmoja wa Ujerumani alikuwa afadhili mradi huo na kisha kuziuza filamu hizo za ngono ulaya.
Vijana hao 21 sasa wamewekwa kwenye karantini ya lazima KMTC ambapo watasalia kwa siku 14.
MHARIRI: DAVIS OJIAMBO