NA NICKSON TOSI

Msanii tajika wa miziki ya injili nchini Mercy Masika amezindua albamu yake mpya kwa jina Zaidi ambayo itakuwa ikipatika katika mtandao wa Boomplay,

Kabla ya uzinduzi huo, Masika na mwanawe wa miaka 10 walianza kuwa na gumzo na mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii.

Baadhi ya nyimbo ambazo amezishirikisha kwenye albamu hiyo ni kama  Zaidi, Nivute, Nitamsifu, Ni Ngutaia’ na  Low Level is Over.

Akitoa albamu hiyo, Masika alisema baadhi ya nyimbo ambazo amezishirikisha ndani ya albamu hiyo zinaangazia maisha yake ya kibinafsi na changamoto ambazo alipitia kabla ya kufanikiwa.

Uzinduzi huo ulijiri wakati ambapo alikuwa anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

View Comments