Baada ya Zari kumuita msanii Diamond deadbeat father, msanii huyo hakukimya bali alimpa bonge la jibu. Hii ni baada ya zari kuposti ujumbe na kusema Diamond hajui wala hana shughuli la kujua wanawe wanavyoendelea.

Diamond akiwa katika mahojiano na runinga ya Wasfi alimwambia Zari kuwa thamani yake katika macho ya Diamond hitawahi kubadilika wala kugeuka.

"Wakatii ambapo umo katika mahusiano na muwe na watoto kuna uchungu ambao unabaki endapo mtawachana na mpenzi wako.

Uchungu huo huwa unawachwa na wanawake kwa maana wao ndio wamebaki na watoto na kuwalea, niliona ujumbe huo na awali tulikuwa tunazungumza kupitia mawakili wetu.

Nilimtumia ujumbe na kumwambia kuwa yeye ni mzazi kama mimi na heshima yake kwangu ndiyo ya maana.'' Alisema Diamond.

Diamond alisema licha na changamoto ambazo wanapitia anamthamini mama wa watoto wake.

''Hii ni kwa sababu alinizalia watoto wangu wa kwanza, na hata tukikosana mara ngapi thamani yake kwa macho yangu haitawahi kubadilika wala kushuka chini.

Nilimwambia hamna haja ya kuposti jumbe zingine kwenye mitandao ya kijamii kwa maana inaleta picha mbaya. Tulizungumza na kila mmoja wetu akatoa shida zake kwenye meza

Na tukagundua kuwa kulikuwa na shida ya mazungumzo kati ya mawakili wetu.'' Aliongea.

Yote tisa kumi akimalizia alikuwa na haya ya kusema,

''Namshukuru  Mola na natumai baada ya janga la corona kusaidiana kulea watoto wetu kutabadilika." Diamond Alizungumza.
View Comments