burburu

Polisi wanachunguza kisa ambacho mwanamume mmoja aliaga dunia kwa kuteketea ndani ya gari lake mtaani Buruburu, Nairobi siku ya Jumanne .

Walinzi wa kibinafsi  waliokuwa  zamuni katika  nyumba za Mai Mahiu Court katika barabara ya Katulo  waliliona gari hilo likiteketea katika eneo la maegesho.

Wazima moto kutoka kaunti ya Nairobi walikimbia kuuzima moto katika gari hilo aina ya Subaru Impreza nambari ya usajili  KBY 779M.

Baada ya kukaguliwa mwili wa mtu huyo uliokuwa umechomeka ulipatikana  na baadaye kutambukiwa kuwa wa mwanamume Terance Korir  mwenye umri wa miaka  36  anayeaminika kuwa mmiliki wa gari hilo.

Marehemu alikuwa akielekeea kazini mwendo wa saa mbili unusu asubuhi wakati wa tukio hilo. Kuna madai kwamba huenda moto huo ulianzishwa na kitakasio lakini hilo halijathibitishwa.  Mwathiriwa amewaacha mkewe na watoto wawiliKO.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO

View Comments