29 April 2020 1 Min Read
Tanzia! Wapenzi wa filamu za Kihindi waomboleza kifo cha Irrfan Khan
by Yusuf Juma Habari
NA NICKSON TOSI
Iwapo wewe ni mtazamaji wa filamu za Kihindi almaarufu kama Action Movies basi hii leo muigizaji mahiri wa filamu hizo Irrfan Khan ameaga dunia hii leo baada ya kulazwa hospitalini Mumbai kwa muda.
Khan alikuwa na matatizo na utumbo wake yaani Colon na kufariki akiwa na miaka 53.
Waigizaji stadi wa filamu za kihindi kama vile Sonam Kapoor, Taapsee Pannu, Bhumi Pednekar, Raveena Tandon na wengine wengi wameelezea kushangazwa na taarifa za kifo cha gwiji huyo .
Kifo chake kinajiri saa chache tu baada ya mamake mzazi kufariki.
Atakumbukwa zaidi kutokana na filamu zake mahiri kama vile Hindi Medium, BlackMail, Inferno, Madaar na nyingine nyingi.